95.Surat At-Tin |
Imeshuka Makka | Ina aya 8 |
Utangulizi | Orodha ya Sura | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Naapa kwa tini na zaituni!
1
2. Na kwa Mlima wa Sinai!
2
3. Na kwa mji huu wenye amani!
3
4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
4
5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
5
6. Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira
usio kwisha.
6
7. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
7
8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?
8
Sura Nyingine | Faharasa |