Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Utangulizi:
Rudi kwenye sura
* 1. Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao.
Rudi kwenye sura
* 2. Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na maraia.
Rudi kwenye sura
* 3. Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.
Rudi kwenye sura
* 4. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi
Mungu dhidi yake.
Rudi kwenye sura
* 5. Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.
Rudi kwenye sura
* 6. Kutokana na majini na wanaadamu.
Rudi kwenye sura
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani