Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Utangulizi:
Rudi kwenye sura
* 1. Naapa kiapo cha mkazo kwa mji wa Makka, mji mtakatifu;
Rudi kwenye sura
* 2. Na wewe unaishi katika mji huu, unauzidisha utukufu wake na cheo chake.
Rudi kwenye sura
* 3. Na naapa kwa mzazi na anacho kizaa, na kwa hao wawili ndio jinsi inahifadhika
na maendeleo yanabakia.
Rudi kwenye sura
* 4. Hakika Sisi tumemuumba mtu katika mashaka na taabu tangu mwanzo wake mpaka
kumalizika mambo yake.
Rudi kwenye sura
* 5. Je! Anadhani mtu aliye umbwa katika mashaka haya kuwa hapana awezae kumdhalilisha?
Rudi kwenye sura
* 6. Anasema: Nimetumia katika kupambana na Muhammad s.a.w. na kuupinga wito wake
mali mengi ukiyakusanya pamoja.
Rudi kwenye sura
* 7. Ati anadhani kwamba mambo yake hayo yamefichikana, hayajui yeyote hata huyo
aliye muumba?
Rudi kwenye sura
* 8,9. Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia, na ulimi na midomo
miwili ili aweze kutamka na kusema sawa?
Rudi kwenye sura
* 8,9. Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia, na ulimi na midomo
miwili ili aweze kutamka na kusema sawa?
Rudi kwenye sura
* 10. Na tukamwonyesha njia ya kheri na ya shari, na tukamtengenezea aweze kuchagua mojawapo?
Rudi kwenye sura
* 11. Basi huyo hakunafiika kwa tuliyo mtengenezea, wala hakuivuka njia ya milimani inayo mzuia
asifikie uwokovu, nayo ni choyo wa nafsi yake.
Rudi kwenye sura
* 12. Na kitu gani kitakufunza nini huko kujitoma kwenye njia ya milimani?
Rudi kwenye sura
* 13. Kumkomboa mtu kutokana na utumwa,
Rudi kwenye sura
* 14. Au kumlisha siku ya njaa
Rudi kwenye sura
* 15. Yatima aliye jamaa wa kumliwaza kwa ujamaa na ufakiri.
Rudi kwenye sura
* 16. Au masikini mwingi wa haja na kufakirika.
Rudi kwenye sura
* 17. Tena awe pamoja na hayo miongoni mwa wenye Imani wanao usiana na
wenzao kwa subira na kuoneana huruma.
Rudi kwenye sura
* 18. Hao wanao sifika kwa sifa hizi, ndio watu wa kheri, wa mkono wa kulia.
Rudi kwenye sura
* 19. Na walio zikataa dalili tulizo zisimamisha kuthibitisha Haki kutoka na
Kitabu na hoja zake, hao ndio wapotovu watu waovu walio kosa kheri na watapata adhabu.
Rudi kwenye sura
* 20. Juu yao utakuwa Moto ulio bebeana na milango yake ikafungwa.
Rudi kwenye sura
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani