104.Surat Al-Humazah |
Imeshuka Makka | Ina aya 9 |
Utangulizi | Sura Nyingine | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0
1. Ole wake kila safihi, msengenyaji! 1
2. Aliye kusanya mali na kuyahisabu. 2
3. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! 3
4. Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. 4
5. Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? 5
6. Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. 6
7. Ambao unapanda nyoyoni. 7
8. Hakika huo utafungiwa nao 8
9. Kwenye nguzo zilio nyooshwa. 9
Sura Nyingine | Faharasa |