37.Suurat Ass 'Affat |
Imeshuka Makka | Ina aya 182 |
Utangulizi | Sura Nyingine | Faharasa |
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0
1. Naapa kwa wanao jipanga kwa safu. 1
2. Na kwa wenye kukataza mabaya. 2
3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho. 3
4. Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. 4
5. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote. 5
6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. 6
7. Na kulinda na kila shet'ani a'si. 7
8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. 8
9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. 9
10. Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara. 10
11. Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata. 11
12. Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara. 12
13. Na wanapo kumbushwa hawakumbuki. 13
14. Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara. 14
15. Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri. 15
16. Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? 16
17. Hata baba zetu wa zamani? 17
18. Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili. 18
19. Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona! 19
20. Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. 20
21. Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha. 21
22. Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu. 22
23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! 23
24. Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa: 24
25. Mna nini? Mbona hamsaidiani? 25
26. Bali hii leo, watasalimu amri. 26
27. Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. 27
28. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. 28
29. Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. 29
30. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. 30
31. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. 31
32. Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. 32
33. Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. 33
34. Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. 34
35. Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna. 35
36. Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? 36
37. Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume. 37
38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. 38
39. Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya. 39
40. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. 40
41. Hao ndio watakao pata riziki maalumu, 41
42. Matunda, nao watahishimiwa. 42
43. Katika Bustani za neema. 43
44. Wako juu ya viti wamekabiliana. 44
45. Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem. 45
46. Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao. 46
47. Hakina madhara, wala hakiwaleweshi. 47
48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. 48
49. Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika. 49
50. Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe. 50
51. Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki. 51
52. Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki. 52
53. Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa? 53
54. Atasema: Je! Nyie mnawaona? 54
55. Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu. 55
56. Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza. 56
57. Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa. 57
58. Je! Sisi hatutakufa, 58
59. Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. 59
60. Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa. 60
61. Kwa mfano wa haya nawatende watendao. 61
62. Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? 62
63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. 63
64. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. 64
65. Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. 65
66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. 66
67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. 67
68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. 68
69. Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. 69
70. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. 70
71. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. 71
72. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. 72
73. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. 73
74. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. 74
75. Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. 75
76. Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa. 76
77. Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia. 77
78. Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye. 78
79. Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote! 79
80. Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. 80
81. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. 81
82. Kisha tukawazamisha wale wengine. 82
83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake, 83
84. Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima. 84
85. Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? 85
86. Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu? 86
87. Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? 87
88. Kisha akapiga jicho kutazama nyota. 88
89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa! 89
90. Nao wakamwacha, wakampa kisogo. 90
91. Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli? 91
92. Mna nini hata hamsemi? 92
93. Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia. 93
94. Basi wakamjia upesi upesi. 94
95. Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe 95
96. ?Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya! 96
97. Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! 97
98. Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini. 98
99. Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa. 99
100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. 100
101. Basi tukambashiria mwana aliye mpole. 101
102. Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. 102
103. Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. 103
104. Tulimwita: Ewe Ibrahim! 104
105. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. 105
106. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri. 106
107. Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. 107
108. Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye. 108
109. Iwe salama kwa Ibrahim! 109
110. Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. 10
111. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. 11
112. Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. 112
113. Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi. 113
114. Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni. 114
115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa. 115
116. Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda. 116
117. Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha. 117
118. Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. 118
119. Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. 119
120. Iwe salama kwa Musa na Haruni! 120
121. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. 121
122. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini. 122
123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. 123
124. Alipo waambia watu wake: Hamwogopi? 124
125. Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji, 125
126. Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani? 126
127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa; 127
128. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. 128
129. Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye. 129
130. Iwe salama kwa Ilyas. 130
131. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. 131
132. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. 132
133. Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. 133
134. Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote, 134
135. Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma. 135
136. Kisha tukawaangamiza wale wengineo. 136
137. Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi, 137
138. Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini? 138
139. Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. 139
140. Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni. 140
141. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa. 141
142. Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa. 142
143. Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu, 143
144. Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa. 144
145. Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. 145
146. Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. 146
147. Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. 147
148. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda. 148
149. Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume? 149
150. Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia? 150
151. Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema: 151
152. Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo! 152
153. Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume? 153
154. Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi? 154
155. Hamkumbuki? 155
156. Au mnayo hoja iliyo wazi? 156
157. Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli. 157
158. Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa. 158
159. Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia. 159
160. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. 160
161. Basi hakika nyinyi na mnao waabudu 161
162. Hamwezi kuwapoteza. 162
163. Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni. 163
164. Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu. 164
165. Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu. 165
166. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa. 166
167. Na walikuwapo walio kuwa wakisema: 167
168. Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani, 168
169. Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi. 169
170. Lakini waliukataa. Basi watakuja jua. 170
171. Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. 171
172. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa. 172
173. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda. 173
174. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda. 174
175. Na watazame, nao wataona. 175
176. Je! Wanaihimiza adhabu yetu? 176
177. Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa. 177
178. Na waache kwa muda. 178
179. Na tazama, na wao wataona. 179
180. Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia. 180
181. Na Salamu juu ya Mitume. 181
182. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. 182
Sura Nyingine | Faharasa |